84. Hadiyth ”Ee msichana wangu kipenzi! Unapoingia msikitini, basi sema… ”

84 – Yahyaa bin ´Abdil-Hamiyd ametuhadithia: Shariyk ametuhadithia, kutoka kwa al-Layth, kutoka kwa ´Abdullaah bin al-Hasan, kutoka kwa mama yake Faatwimah bint al-Husayn, kutoka kwa Faatwimah, msichana wa Mtume (Swalla Allâhu ´alayhi wa sallam), kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mfano wake[1].

[1] Cheni ya wapokezi ni dhaifu kwa sababu ya Yahyaa al-Himaaniy, Shariyk bin ´Abdillaah al-Qaadhwiy na Layth bin Abiy Sulaym – wote ni wanyonge. Hata hivyo Hadiyth imesimuliwa kwa njia nyingine. Ameipokea at-Tirmidhiy, Ahmad na Ibn Maajah ameipokea kupitia kwa Ismaa´iyl bin Ibraahiym, kutoka kwa Layth. Lakini Hadiyth inajulisha kitendo chake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na si maneno yake. Tamko la Hadiyth ni:

”Alikuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anapoingia msikitini, basi anamswalia na kumtakia amani Muhammad na kusema:

رب اغفر لي ذنوبي و افتح لي أبواب رحمتك

”Ee Mola! Nisamehe madhambi yangu na nifungulie milango ya rehema Zako.”

Wakati anapotoka anamswalia na kumtakia amani Muhammad na kusema:

رب اغفر لي ذنوبي و افتح لي أبواب فضلك

”Ee Mola! Nisamehe madhambi yangu na nifungulie milango ya fadhilah Zako.”

at-Tirmidhiy na Ahmad wamezidisha:

”Ismaa´iyl bin Ibraahiym amesema: ”Nikakutana na ´Abdullaah bin Hasan Makkah na nikamuuliza juu ya Hadiyth hii. Akanihadithia: ”Pindi anapoingia, alikuwa akisema:

رب افتح لي باب رحمتك

”Ee Mola! Nifungulie mlango wa rehema Zako.”

Pindi anapotoka husema:

رب افتح لي باب فضلك

”Ee Mola! Nifungulie mlango wa fadhilah Zako.”

Huu ni ufuatiliaji wenye nguvu kutoka kwa Ismaa´iyl bin Ibraahiym bin ´Ulayyah, ambaye ni mwaminifu. Kwa hivyo cheni ya wapokezi ikasalimika kutokana na baadhi ya wapokezi wake. Tayari kumeshatangulia ufuatiliaji mwingine (82), lakini kwa cheni ya wapokezi ambayo inahitaji kuangaliwa vyema. Kasoro katika cheni ya wapokezi ni kukatika. Kasoro hiyo imetajwa na at-Tirmidhiy wakati aliposema:

”Hadiyth ya Faatwimah ni nzuri, lakini cheni ya wapokezi haikuungana. Faatwimah bint al-Husayn hakuwahi kukutana na Faatwimah (Radhiya Allaahu ´anhaa), kwa sababu Faatwimah huyu wa pili aliishi miezi kadhaa tu baada ya kufa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 75
  • Imechapishwa: 07/02/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy