83. Hadiyth ”Ee msichana wangu kipenzi! Unapoingia msikitini, basi sema… ”

83 – Yahyaa ametuhadithia: Qays ametuhadithia, kutoka kwa ´Abdullaah bin al-Hasan, kutoka kwa mama yake Faatwimah bint al-Husayn, kutoka kwa Faatwimah, msichana wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alinambia: ”Ee msichana wangu kipenzi! Unapoingia msikitini, basi sema:

بسم الله، و السلام على رسول الله، اللهم صل على محمد و على آل محمد، اللهم اغفر لنا و ارحمنا و افتح لنا أبواب رحمتك

”Kwa jina la Allaah. Amani iwe juu ya Mtume wa Allaah. Ee Allaah! Msifu Muhammad na jamaa zake Muhammad. Ee Allaah! Tusamehe, uturehemu na utufungulie milango ya rehema Zako.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi ni dhaifu. Wapokezi wake wamekwishatangulia, mbali na Qays bin ar-Rabiy´, ambaye ni mnyonge.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 75
  • Imechapishwa: 07/02/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy