82. Hadiyth ”Unapoingia msikitini, basi sema… ”

82 – Yahyaa bin ´Abdil-Hamiyd ametuhadithia: ´Abdul-´Aziyz bin Muhammad ametuhadithia, kutoka kwa ´Abdullaah bin al-Hasan, kutoka kwa mama yake Faatwimah bint al-Husayn, kutoka kwa Faatwimah, msichana wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye ameeleza:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alinambia: ”Unapoingia msikitini, basi sema:

بسم الله، و السلام على رسول الله، اللهم صل على محمد و على آل محمد، و اغفر لنا، و سهل لنا أبواب رحمتك

”Kwa jina la Allaah. Amani iwe juu ya Mtume wa Allaah. Ee Allaah! Msifu Muhammad na jamaa zake Muhammad. Tusamehe na utusahilishie milango ya rehema Zako.”

Ukimaliza, basi sema vivyo hivyo isipokuwa tu:

و سهل لنا أبواب فضلك

”… na utusahilishie milango ya rehema Zako.”[1]

[1] Swahiyh kupitia mapokezi mengine yanayoitia nguvu. Yahya abin ´Abdil-Hamiyd ni al-Himaaniy, na jambo lake limekwishatangulia kutajwa. Wapokezi wengine ni waaminifu. Lakini cheni ya wapokezi imekatika, kama itakavyokuja huko mbele. Kama ilivyo katika “Jalaal-ul-Afhaam”, uk. 52, Hadiyth ameipokea Abul-´Abbaas ath-Thaqafiy kupitia kwa Qutaybah bin Sa´iyd: ´Abdul-´Aziyz ametuhadithia…

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 73-74
  • Imechapishwa: 07/02/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy