Kusimama kuswali usiku wa kuamkia ijumaa 02

Swali: Je, inajuzu kufanya maalum usiku wa kuamkia ijumaa mtu akasimama usiku pamoja na kuzingatia ya kwamba sisi ni wanafunzi na wengine ni wafanyakazi? Jengine ni kwa sababu tutumie fursa ya likizo ya siku ya ijumaa ambapo tumetulia. Kwa sababu kuna ndugu mmoja aliyesema kwamba kuna Hadiyth inayofahamisha kwamba haifai kufanya maalum mchana au usiku wowote kwa ajili ya ´ibaadah. Tunatarajia fatwa yako na Allaah akujaze kheri.

Jibu: Ndio, haijuzu kufanya maalum usiku wa kuamkia ijumaa mtu akasimama usiku. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kufanya hivo. Kama ambavyo vilevile haijuzu kufanya mchana wake maalum kwa kufunga. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Msifanye maalum mchana wa ijumaa kwa kufunga isipokuwa ile swawm ambayo mmoja wenu amezowea kufunga na wala msifanye maalum usiku wa kuamkia ijumaa kwa kusimama usiku.”

Kwa hivyo haifai kwa mtu kuufanya maalum kwa kusimama usiku wala mchana wake kwa kufunga. Vivyo hivyo haijuzu kufanya usiku wowote maalum ambapo mtu akawa anaswali swalah za usiku. Hakuna dalili ya kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/11925/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%AA%D8%AE%D8%B5%D9%8A%D8%B5-%D9%84%D9%8A%D9%84%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D8%AC%D9%85%D8%B9%D8%A9-%D8%A8%D9%82%D9%8A%D8%A7%D9%85
  • Imechapishwa: 18/12/2018