Kusimama kwa ajili ya mtumzima

Swali: Je, kumepokelewa kitu kuhusu kusimama kwa ajili ya mtumzima? Je, kufanya hivo ni heshima?

Jibu: Hapana vibaya kusimama kwa ajili yake na kupeana mkono. Wakati Ka´b bin Maalik alipoingia baada ya Allaah kumkubalia tawbah yake basi Twalhah bin ´Ubaydillaah alimsimamia kwa ajili ya kumkimbilia na kumpa mkono. Aidha wakati Sa´d bin Mu´aadh alipokuja ili ahukumu kati ya Banuu Quraydhwah Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema:

“Simameni kwa ajili ya bwana wenu.”

Walisimama kwa ajili yake, wakapeana mkono na wakamshusha kutoka katika kipando chake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23348/هل-يجوز-القيام-للشخص-لسنه-او-مكانته
  • Imechapishwa: 30/12/2023