Kurefusha Sujuud zaidi kuliko kisimamo katika swalah inayopendeza

Swali: Anayeswali swalah inayopendeza arefushe Sujuud kuliko anavyorefusha kisimamo?

Jibu: Hapana, swalah yake iwe ya kati na kati. al-Baraa´ (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza:

“Nimetazama swalah yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuona kisimamo chake, Rukuu´ yake, kuinuka kwake kutoka katika Rukuu´, Sujuud yake na kikao chake kati ya sijda mbili vinakaribiana.”

Kwa maana nyingine swalah yake inakuwa wastani na yenye kukaribiana.

Swali: Je, akemewe anayefanya hivo?

Jibu: Jambo ni lenye wasaa. Hakuna kukemeana. Jambo ni lenye wasaa. Mtu asifanye ugumu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22627/حكم-اطالة-سجود-النافلة-اكثر-من-القيام
  • Imechapishwa: 14/07/2023