Swali: Mtu aseme nini baada ya Rukuu´ pale anapokuwa amesimama kunyooka sawasawa?

Jibu: Aseme:

رَبَّنَا وَلَكَ الْحَمْدُ، حَمْداً كَثيراً طَيِّباً مُبارَكاً فِيهِ أَهلَ الثَّناءِ وَالْمَجْدِ، أَحَقُّ مَا قَالَ الْعَبْدُ، وَكُلُّنَا لَكَ عَبْدٌ. اللَّهُمَّ لاَ مَانِعَ لِمَاأَعْطَيْتَ، وَلاَ مُعْطِيَ لِمَا مَنَعْتَ، وَلاَ يَنْفَعُ ذَا الجَدِّ مِنْكَ الجَدُّ

“Ee Mola wetu, sifa zote njema ni Zako, sifa nyingi, nzuri na zilizobarikiwa ndani yake. Wewe ni mstahiki wa sifa na utukufu, ni ukweli yale yaliyosemwa na mja, na sisi wote Kwako ni waja. Ee Allaah! Hapana awezaye kukizuia kile Ulichokitoa na hapana awezaye kukitoa kile Ulichokizuia na wala haumnufaishi mwenye utajiri, kwani Kwako Wewe ndiko kunatoka utajiri.”[1]

Akariri himdi na sifa. Baina ya Sujuud mbili aseme:

رب اغفر لي، رب اغفر لي

“Ee Mola! Nisamehe! Ee Mola! Nisamehe!”

Akariri:

اللهم اغفر وارحمني واهدني واجبرني وارزقني

“Ee Allaah! Nisamehe, unirehemu, uniongoze, uniunge na uniruzuku.”

اللهم اغفر لي وارحمني، اللهم أصلح قلبي وعملي، اللهم اغفر لي ولوالدي

“Ee Allaah! Nisamehe na unirehemu. Ee Allaah! Utengeneze moyo wangu. Ee Allaah! Nisemehe mimi na wazazi wangu.”

Akariri du´aa.

[1] Muslim (477).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22630/ما-يقال-في-الرفع-من-الركوع-وبين-السجدتين
  • Imechapishwa: 14/07/2023