Kupeana mkono na aliyeingia mahali walipo watu

Swali: Wakati Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa anaingia mahali walipo Maswahabah zake nao wamekaa alikuwa akiwasalimia kwa kupeana nao mkono au anawatolea salamu kisha anakaa pale kinapoishia kikao?

Jibu: Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiketi pale kinapoishilia kikao.

Swali: Akipeana nao mkono?

Jibu: Hatujafikiwa na hilo. Maswahabah walikuwa wanapeana mkono pindi wanapokutana na anapoingia basi hawasimami kwa ajili yake. Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaketi pale kinapoishia kikao.

Swali: Hadiyth inayozungumzia kupeana mkono?

Jibu: Ni Sunnah. Wakipeana mkono ni Sunnah. Lakini hatukufikiwa na khabari kuwa walikuwa wakisimama kwa ajili yake na kupeana mkono. Kwa sababu kitendo hicho kinaweza kuwakalifisha watu sana.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22240/حكم-المصافحة-لمن-دخل-على-قوم-جلوس
  • Imechapishwa: 19/01/2023