Kuoa kwa nia ya talaka ni kumhadaa mwanamke

Swali: Ipi hukumu ya kuoa kwa nia ya kuacha na ni kama Mut´ah?

Jibu: Kuoa kwa nia ya kuacha sio kama Mut´ah. Kuna tofauti. Lakini hata hivyo maoni ya sahihi ni kwamba haijuzu. Kwa kuwa ni kumhadaa mwanamke, [haikukatazwa] kwa sababu ni kama Mut´ah isipokuwa ni kwa sababu ni kumghuri mwanamke na walii wake. Kwa sababu wewe umemuoa kwa nia ya kuishi naye ilihali wewe unaficha ndani ya nafsi yako nia ya [… sauti imepotea… ]. Ni Mut´ah iliyojificha na sio Mut´ah ya waziwazi […]. Itakuwa Mut´ah kwa wale ambao watanuia mwanamke na walii. Kwa hivyo hii haiitwi Mut´ah ya kihakika.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.alfawzan.af.org.sa/alldroos?tid_1=164
  • Imechapishwa: 19/01/2023