Kupangusa mwili baada ya Adhkaar za asubuhi na jioni

Swali: Je, imethibiti Muislamu baada ya kusoma kwake Adhkaar za asubuhi na jioni apulize kwenye mikono yake kisha apanguse kwa mikono yake mwili wake mzima?

Jibu: Hili ni wakati wa kulala. Hili limethibiti wakati wa kulala ndio anatakiwa kusoma Suurah tatu; al-Ikhlaasw, an-Naas na al-Falaq kisha apanguse mwili wake, kama alivyokuwa akifanya (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ama nyuradi, hapana, halikuthibiti kutokana na ninavyojua.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (31) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1430-10-9.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020