Swalah ya mkusanyiko ya mume na mke

Swali: Ni lipi bora kwa mwanaume anapopitwa na swalah ya mkusanyiko; aswali peke yake au aswali na mke wake? Akiswali na mke wake anapata ujira wa mkusanyiko?

Jibu: Swalah ya mkusanyiko haipatikani isipokuwa kwa wanaume wawili na zaidi. Haipatikani kwa mwanaume mmoja na mwanamke. Lakini mke wako akiswali pamoja na wewe kwa minajili ya kukufuata ni sawa. Ama kusema kuwa unapata mkusanyiko sijui hilo. Swalah ya mkusanyiko inakuwa kwa wanaume wawili na zaidi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (31) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1430-10-9.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020