Mama anatakiwa awe mkali katika mambo ya dini

Swali: Mimi ni mwanamke mwenye msimamo katika dini ya Allaah. Nina watoto wasioswali na wanasikiliza nyimbo. Nimewanasihi mara nyingi lakini pasi na mafanikio yoyote. Wakati mwingine ninakuwa mgumu kwao. Je, ninapata dhambi kwa ugumu huu? Unaninasihi nini?

Jibu: Ninakunasihi kuomba msaada kutoka kwa Allaah na uendelee kuwanasihi. Mambo yakihitajia kuwa mgumu ni sawa. Ugumu huu ni kwa ajili ya dini ya Allaah na kwa ajili waathirike na waache yale waliyomo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (31) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1430-10-9.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020