Kupandikiza moyo wa kafiri kwenye mwili wa muislamu

Swali: Ni ipi hukumu ya kufanya upasuaji hospitali kwa ajili ya kupandikiza moyo wa kafiri kwenye mwili wa muumini?

Jibu: Wanazuoni wamekinzana juu ya jambo hili. Hapana vibaya kuupandikiza. Akimtii Allaah na akamtakasia nia, basi moyo huo umehama kutoka katika moyo wa kafiri na kwenda katika moyo wa muumini. Ni kama ambavyo vinahamishwa vidole, mkono au jino lake.

Swali: Hukumu hii ni maalum kwa ambaye ni kafiri?

Jibu: Ndio, pindi muumini anapohitaji kiungo cha kafiri.

Swali: Imani inakuweje katika hali kama hii?

Jibu: Imani maeneo pake ni moyoni. Kumcha Allaah, kumpenda Allaah na kumtakasia nia Allaah kunahama kutoka katika hali mbaya na kwenda katika hali nzuri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22182/حكم-زراعة-قلب-الكافر-في-جسد-المومن
  • Imechapishwa: 01/11/2022