Kuhangaika na dunia kwa ajili ya kuwafanyia watu wema

Swali: Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema kuwa mwenye kuitafuta dunia kwa lengo la kuwafanyia watu wema basi shaytwaan anakuwa mwenye kumpendezeshea nayo na hivyo anatumbukia katika kuipenda dunia na kujishughulisha nayo.

Jibu: Haidhuru akitafuta riziki. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Pupia yale yenye kukunufaisha.”

Akikusudia kutoa swadaqah, kufanya wema na kuwanufaisha watu ni mwenye kulipwa thawabu. Hivyo ndivo alivofanya as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye alijitolea mali yake kwa ajili ya kuinusuru dini na kumuhami Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumhudumia. Vivyo hivyo ´Umar alijitolea mali yake. Vilevile ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf na Maswahabah wengine matajiri. Allaah aliwanufaisha waislamu kupitia wao.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22185/هل-يجوز-طلب-الدنيا-بنية-الاحسان-للناس
  • Imechapishwa: 01/11/2022