Imaam Ibn Qudaamah (Rahimahu Allaah) amesema:

Miongoni mwa sifa za Allaah (Ta´ala) ni kuwa anafanya kile anachokitaka. Hakiwi kitu isipokuwa kwa kutaka Kwake na wala hakitoki kitu nje ya utashi Wake. Hakuna kitu ulimwenguni kinachotoka nje ya makadirio Yake wala nje ya uendeshaji Wake. Haiwezekani kuepuka Qadar iliyokadiriwa na wala haiwezi mtu hawezi kuvuka yaliyoandikwa katika Ubao uliohifadhiwa. Viumbe wote hutenda kwa matakwa Yake. Lau angeliwalinda wasingemkhalifu. Lau angelitaka wote wamtii basi wangelimtii. Kaumba viumbe na matendo yao na amekadiria riziki zao na muda wao wa kueshi. Anamwongoza amtakaye kwa rehema Zake na anampoteza amtakaye kwa hekima Yake. Allaah (Ta´ala) amesema:

لَا يُسْأَلُ عَمَّا يَفْعَلُ وَهُمْ يُسْأَلُونَ

“Haulizwi kwa yale Anayoyafanya, lakini wao wataulizwa.”[1]

إِنَّا كُلَّ شَيْءٍ خَلَقْنَاهُ بِقَدَرٍ

”Hakika Sisi tumekiumba kila kitu kwa makadirio.”[2]

وَخَلَقَ كُلَّ شَيْءٍ فَقَدَّرَهُ تَقْدِيرًا

”Ameumba kila kitu kisha akakikadiria kipimo sawasawa.”[3]

مَا أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي أَنفُسِكُمْ إِلَّا فِي كِتَابٍ مِّن قَبْلِ أَن نَّبْرَأَهَا

 “Hakuna msiba wowote unaokusibuni katika ardhi au katika nafsi zenu isipokuwa umo katika Kitabu kabla Hatujauumba.”[4]

فَمَن يُرِدِ اللَّـهُ أَن يَهْدِيَهُ يَشْرَحْ صَدْرَهُ لِلْإِسْلَامِ ۖ وَمَن يُرِدْ أَن يُضِلَّهُ يَجْعَلْ صَدْرَهُ ضَيِّقًا حَرَجًا

”Basi yule ambaye Allaah anataka kumwongoza basi humfungulia kifua chake kwa Uislamu. Na yule ambaye anataka kumpoteza humjaalia kifua chake kuwa na dhiki chenye kubana.”[5]

Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amepokea ya kwamba Jibriyl (´alayhis-Salaam) alimuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Nambie kuhusu imani?” Akasema: “Ni kumuamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Mitume Yake, siku ya Mwisho na kheri na shari ya Qadar.” Jibriyl akamwambia: “Umesema kweli.”[6] Imepokelewa na Muslim.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Naamini Qadar; kheri na shari yake, mazuri na machungu yake.”[7]

Miongoni mwa du´aa za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambazo alimfunza al-Hasan bin ´Aliy aombe katika Qunuut ya Witr ni ifuatayo:

وقني شر ما قضيت

“Nikinge na shari ya Uliyokadiria.”[8]

MAELEZO

Miongoni mwa sifa Zake (Ta´ala) ni kwamba ni mwenye kufanya akitakacho. Amesema (Ta´ala):

إِنَّ رَبَّكَ فَعَّالٌ لِّمَا يُرِيدُ

“Hakika Mola wako anafanya atakavyo.”[9]

Hakitoki kitu nje ya matakwa na ufalme Wake na wala hakifanyiki kitu isipokuwa kwa maendesho na kipimo Chake. Mkononi Mwake kuna ufalme wa mbingu na ardhi. Anamwongoza amtakaye kwa rehema na anampotosha amtakaye kwa hekima Yake. Haulizwi kutokana na yale anayoyafanya kutokana na ukamilifu wa hekima na ufalme Wake. Lakini wao wataulizwa kwa sababu ni wenye kuendeshwa na wenye kuhukumiwa.

Kuamini makadirio ni lazima. Ni moja miongoni mwa zile nguzo za imani. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ni kumuamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Mitume Yake, siku ya Mwisho na kheri na shari ya Qadar.” Jibriyl akamwambia: “Umesema kweli.”

Ameipokea Muslim.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Naamini Qadar; kheri na shari yake, mazuri na machungu yake.”

Kheri na shari ni kwa kuzingatia ule mwisho na matokeo yake. Utamu na uchungu wake ni kwa kuzingatia ule wakati wa kumgonga kwake mtu. Kheri ya makadirio ni kutokana na kule kunufaisha kwake na shari yake ni kutokana na kule kudhuru au kuudhi kwake. Kheri na shari ni kwa kuzingatia kile kilichokadiriwa na ule mwisho wake. Kuna ambayo inakuwa ni kheri; kama vile utiifu, uzima na utajiri. Kuna ambayo inakuwa ni shari; kama vile maasi, ugonjwa na umasikini. Lakini kwa kuzingatia kitendo cha Allaah hakusemwi kuwa ni shari. Hilo ni kutokana na maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika du´aa ya Qunuut ambayo alimfunza al-Hasan bin ´Aliy:

وقني شر ما قضيت

“Nikinge na shari ya Uliyokadiria.”[10]

Ameegemeza shari katika aliyoyakadiria na si katika makadirio Yake Yeye.

[1] 21:23

[2] 54:49

[3] 25:02

[4] 57:22

[5] 06:125

[6] al-Bukhaariy (50) na (4777) na Muslim (8).

[7] al-Haakim katika ”Ma´rifah ´Uluum-il-Hadiyth” (31) na (32). Tanbihi muhimu! Cheni ya wapokezi ni dhaifu. Katika cheni ya wapokezi yuko Yaziyd ar-Ruqaashiy na ni mnyonge, na hilo limetajwa katika ”at-Taqriyb” (7683). Imaam an-Nasaa´iy (Rahimahu Allaah) amesema juu yake: ”Ni mwenye kuachwa.”, na Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amesema: ”Hadiyth ni munkari.” na hilo limetajwa katika ”al-Miyzaan” (4/418).

[8] Ahmad (1723), Abu Daawuud (1425) na (1426), at-Tirmidhiy (464), an-Nasaa´iy (3/248) na Ibn Maajah (1178). Shaykh Ahmad Shaakir (Rahimahu Allaah) amesema kuwa ni Swahiyh katika maelezo yake ya “Sunan at-Tirmidhiy”.

Faida muhimu!

Shaykh Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn amesema katika darsa za fataawaa zake za msikiti Mtakatifu wa Makkah mwaka wa 1408, uk. 136 akifafanua du´aa ya Qunuut: Maneno yake:

وقني شر ما قضيت

“Nikinge na shari ya Uliyokadiria.”

Allaah (´Azza wa Jall) anakadiria kwa yaliyo na kheri na anakadiria kwa yaliyo na shari. Kuhusu kukadiria Kwake kheri inakuwa kheri tupu juu ya qadar na yule anayefanyiwa qadar hiyo. Mfano wa hilo Allaah (´Azza wa Jall) awakadirie watu riziki kunjufu, amani, utulivu, uongofu na kunusuriwa… Haya ni kheri juu ya qadar na yule anayefanyiwa qadar hiyo. Lakini kukadiria Kwake shari inakuwa ni kheri juu ya ile qadar lakini shari kwa yule mfanyiwaji. Mfano wa hilo ni ukame na ukosefu wa mvua. Haya ni shari. Lakini kule Allaah kuyakadiria ni kheri. Amesema (Ta´ala):

ظَهَرَ الْفَسَادُ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ بِمَا كَسَبَتْ أَيْدِي النَّاسِ لِيُذِيقَهُم بَعْضَ الَّذِي عَمِلُوا لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ

“Ufisadi umedhihiri katika nchi kavu na baharini kwa sababu ya yale iliyochuma mikono ya watu ili awaonjeshe baadhi ya ambayo wameyatenda ili wapate kurejea.” (30:41)

Uharibifu huu una lengo zuri; kurejea kwa Allaah (Ta´ala) kutokana na kumuasi na badala yake watu wa wamtii. Kwa hiyo kile kilichokadiriwa kinakuwa ni shari lakini makadirio yenyewe kama yenyewe yanakuwa ni kheri. Sisi tunasema:

شر ما قضيت

“… shari ya Uliyokadiria.”

Bi maana shari Uliyokadiria Wewe. Allaah (Ta´ala) anaweza kukadiria shari kwa hekima kubwa na yenye kusifiwa.”

[9] 11:107

[10] Ahmad (1723), Abu Daawuud (1425) na (1426), at-Tirmidhiy (464), an-Nasaa´iy (3/248) na Ibn Maajah (1178). Shaykh Ahmad Shaakir (Rahimahu Allaah) amesema kuwa ni Swahiyh katika maelezo yake ya “Sunan at-Tirmidhiy”.

Faida muhimu!

Shaykh Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn amesema katika darsa za fataawaa zake za msikiti Mtakatifu wa Makkah mwaka wa 1408, uk. 136 akifafanua du´aa ya Qunuut: Maneno yake:

وقني شر ما قضيت

“Nikinge na shari ya Uliyokadiria.”

Allaah (´Azza wa Jall) anakadiria kwa yaliyo na kheri na anakadiria kwa yaliyo na shari. Kuhusu kukadiria Kwake kheri inakuwa kheri tupu juu ya qadar na yule anayefanyiwa qadar hiyo. Mfano wa hilo Allaah (´Azza wa Jall) awakadirie watu riziki kunjufu, amani, utulivu, uongofu na kunusuriwa… Haya ni kheri juu ya qadar na yule anayefanyiwa qadar hiyo. Lakini kukadiria Kwake shari inakuwa ni kheri juu ya ile qadar lakini shari kwa yule mfanyiwaji. Mfano wa hilo ni ukame na ukosefu wa mvua. Haya ni shari. Lakini kule Allaah kuyakadiria ni kheri. Amesema (Ta´ala):

ظَهَرَ الْفَسَادُ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ بِمَا كَسَبَتْ أَيْدِي النَّاسِ لِيُذِيقَهُم بَعْضَ الَّذِي عَمِلُوا لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ

“Ufisadi umedhihiri katika nchi kavu na baharini kwa sababu ya yale iliyochuma mikono ya watu ili awaonjeshe baadhi ya ambayo wameyatenda ili wapate kurejea.” (30:41)

Uharibifu huu una lengo zuri; kurejea kwa Allaah (Ta´ala) kutokana na kumuasi na badala yake watu wa wamtii. Kwa hiyo kile kilichokadiriwa kinakuwa ni shari lakini makadirio yenyewe kama yenyewe yanakuwa ni kheri. Sisi tunasema:

شر ما قضيت

“… shari ya Uliyokadiria.”

Bi maana shari Uliyokadiria Wewe. Allaah (Ta´ala) anaweza kukadiria shari kwa hekima kubwa na yenye kusifiwa.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 87-92
  • Imechapishwa: 01/11/2022