Swali: Vipi kuhusu [mswaliji] kuondoka kabla ya kugeuka kwa imamu?
Jibu: Hapana vibaya. Akitoa salamu swalah imemalizika. Lakini bora aketi chini hadi amalize kusema:
أستغفر الله
“Allaah nisamehe.”
Mara tatu.
واللهم أنت السلام ومنك السلام تباركت يا ذا الجلال والإكرام
“Ee Allaah! Wewe ndiye as-Salaam, amani inatoka Kwako, umebarikika, Ee Mwenye utukufu na ukarimu.”
Baada ya hapo asome zile Adhkaar zilizowekwa katika Shari´ah. Hivi ndio bora. Vinginevyo akitoa salamu swalah imemalizika.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23039/حكم-انصراف-الماموم-قبل-ان-ينصرف-الامام
- Imechapishwa: 20/10/2023