54. Makubaliano ya amani ya Hudaybiyah yalikuweje?

Swali 54: Makubaliano ya amani ya Hudaybiyah yalikuweje?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Quraysh walikubaliana kusimamisha vita miaka kumi. Mkataba huo ulikuwa unasema waislamu wote wanaokuja kutoka kwa washirikina wanatakiwa kumrudisha, lakini wale washirikina wanaokuja kutoka kwa waislamu watabaki kwa washirikina. Ambaye atataka kuingia ndani ya makubaliano ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) atafanya hivo, na ambaye atataka kuingia ndani ya makubaliano ya Quraysh atafanya hivo. Hivyo Khuzaa´ah wakajiunga kwenye mafungamano ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), na Banuu Bakr wakajiunga kwenye makubaliano ya Quraysh. Sharti nyingine ilikuwa kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na waislamu warudi na hawatoingia Makkah mwaka huo, na kwamba watafanya ´Umrah mwaka unaofuata. Kisha washirikina ilikuwa watoke Makkah kwa muda wa siku tatu kisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) atoke kwenye mji. Makubaliano hayo yakapigwa muhuri juu ya masharti hayo ambapo kukateremshwa juu yake Suurah ”al-Fath”. Kwa hiyo makubaliano hayo ya amani yakawa ni ushindi wa haraka.

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 117-118
  • Imechapishwa: 20/10/2023