Swali: Je, anapata dhambi ambaye amehifadhi Qur-aan kisha akasahau kwa kupuuza?

Jibu: Kunakhofiwa juu yake. Lakini sahihi ni kwamba hapati dhambi kwa kule kusahau peke yake. Allaah anasema:

رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا

“Ee Mola wetu! Usituchukulie pale tutaposahau au tukikosea.”[1]

Lakini anapaswa kujitahidi, kupupia na kudumu katika kusoma ili asisahau.

[1] 02:286

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23037/حكم-من-حفظ-القران-ثم-نسيه-تهاونا
  • Imechapishwa: 20/10/2023