Kuomba mwa haki ya majina na sifa za Allaah

Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kusema:

“Ee Allaah! Ninakuomba kwa haki ya majina Yako Kwako?”

Jibu: Hili halina msingi. Je, majina ya Allaah yana haki mbele ya Allaah? Nani amesema hivi? Badala yake sema:

“Ee Allaah! Ninakuomba kwa majina Yako.”

pasi na kusema:

“… kwa haki ya majina Yako.”

Sema:

“Ee Allaah Ninakuomba kwa majina na sifa Zako.”

Hili ndio limethibiti. Amesema (Ta´ala):

وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا

“Allaah ana majina mazuri kabisa, basi muombeni kwayo.” (07:180)

Hakusema:

“Ombeni kwa haki zake [majina hayo].”

Tusizushe kitu kutoka kwetu wenyewe.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (31) http://alfawzan.af.org.sa/node/2143
  • Imechapishwa: 12/07/2020