Swalah kwenye misikiti ya makaburi

Swali: Katika mji wangu misikiti mingi ina makaburi. Je, swalah inasihi kwenye misikiti hii kwa nisba yetu?

Jibu: Hapana. Swalah haisihi kwenye makaburi, ni mamoja yakiwa kwenye misikiti au nje ya misikiti. Usiswali kwenye makaburi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kuswali kwenye makaburi na kuyafanya ni mahala pa kuswalia. Hii ni njia inayopelekea katika shirki. Makatazo yanapelekea katika kuharibika. Swali kwenye msikiti usiokuwa na makaburi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (31) http://alfawzan.af.org.sa/node/2143
  • Imechapishwa: 12/07/2020