Swali: Je, kufanya ndoa Sha´abaan na baada ya ´Aswr ni katika Sunnah?
Jibu: Ndoa Sha´abaan ni mubaha , hakuna fadhila maalum. Fadhilah zimekuja kuoa baina ya ´iyd mbili, Mtume (´alayhis-Salaam) alimuoa ´Aaishah au kwa maana hii baina ya ´iyd mbili. Kadiri utavyoweza, ni mamoja ikiwa ni Shawwal au Dhul-Qa’dah. Ama mbali na hiyo miezi ni mubaha isipokuwa tu wakati wa Ihraam. Ikiwa wewe ni Muhrim , sawa ikiwa ni Hajj au ´Umrah haijuzu kufanya ndoa. Wala haijuzu kuchumbia wala kuchumbiwa, kwa kuwa ni Muhrim. Lakini kwa mtu ambae si Muhrim wakati wowote anaweza kuoa au kuolewa.
Swali: Kuoa baada ya ´Aswr?
Jibu: Hakuna kitu. Wakati wowote sawa usiku au mchana mtu anaweza kufanya ndoa.
- Muhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Waswaabiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=2457
- Imechapishwa: 22/09/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)