Kunajisika kwa mavazi aliyovaa mwanamke wakati wa hedhi

Swali: Mwanamke akiwa na hedhi kisha akatoka kwenda kuwatembelea baadhi ya marafiki zake na akavaa moja katika kanzu zake maalum kwa ajili ya matembezi. Aliporudi akavua kanzu hii. Kisha alipotwahirika akaivaa kanzu hii kwa mara nyingine ambapo mara ya kwanza alikuwa na ada yake ya mwezi. Je, kanzu hii inakuwa najisi au hapana?

Jibu: Kanzu hii haiwi najisi isipokuwa kama iliguswa na damu ya hedhi. Ikipatwa na damu ya hedhi basi anatakiwa kuosha damu hiyo. Hivo ndivo alivyoamrisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati alipoulizwa juu ya damu ya hedhi inayoingia kwenye nguo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:

”Ataipikicha, kisha ataikwangua kwa ncha za vidole na maji, kisha atainyunyizia maji na kisha ataswalia.”

Au alisema:

“Kisha aioshe halafu ataswalia.”

Kanzu hii aliyovaa ikiwa haikuguswa na damu basi ni safi na inafaa kuswali nayo. Ikipatwa na damu basi damu hiyo itaoshwa na ataswali nayo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (16) http://binothaimeen.net/content/6813
  • Imechapishwa: 10/09/2021