Kuna tamko maalum kwa ajili ya kupongezana ´Iyd-ul-Adhwhaa?

Swali: Ni ipi namna ya kupongezana kwa ajili ya ´Iyd-ul-Adhwhaa iliyobarikiwa? Tumekwishatangulia kwamba siku ya ´Iyd-ul-Fitwr watu huambizana:

تقبل الله منا ومنكم صالح الأعمال

“Allaah atutakabalie matendo yetu mema sisi na nyinyi.”

Tuseme nini kuhusu ´Iyd-ul-Adhwhaa?

Jibu: Kitu hiki hakina namna maalum. Akimwombea du´aa kwa kusema:

تقبل الله منا ومنكم

“Allaah atutakabalie sisi na nyinyi.”

عيدكم مبارك

“[Nakutakieni] sikukuu yenu iliyobarikiwa.”

العيد مبارك

“[Nakutakieni] sikukuu iliyobarikiwa.”

جعل الله عيدكم مباركًا

“Allaah afanye sikukuu yenu ni yenye kubarikiwa.”

Ni mamoja ni ´Iyd-ul-Adhwhaa au ´Iyd-ul-Fitwr. Zote ni moja. Vivyo hivyo kuhusu hajj:

حجك مقبول

“Hija yako yenye kukubaliwa.”

تقبل الله منك

“Allaah akukubalie.”

عمرة مقبولة

“´Umrah yenye kukubaliwa.”

تقبل الله منك

“Allaah akukubalie.”

Zote hizi na mfano wake ni zenye kutosha. Tunamuomba Allaah atuongoze na kutuwafikisha sote.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/18428/صفة-التهنىة-بالعيد
  • Imechapishwa: 30/04/2022