Swali: Watu siku ya ´Iyd huambizana:

تقبل الله منا ومنكم الأعمال الصالحة

 “Allaah atutakabalie matendo yetu mema sisi na nyinyi.”

Je, si ni bora mtu aombe du´aa ya kukubaliwa matendo yote? Je, kuna du´aa iliyowekwa katika Shari´ah katika mnasaba kama huu?

Jibu: Hapana neno muislamu akamwambia nduguye siku ya ´Iyd au siku nyingine:

تقبل الله منا ومنك أعمالنا الصالحة

“Allaah atutakabalie matendo yetu mema sisi na nyinyi.”

Sitambui juu ya hili kitu maalum. Hakika si venginevyo muumini amwombee ndugu yake du´aa nzurinzuri kutokana na dalili nyingi zilizopokelewa juu ya hilo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (13/25)
  • Imechapishwa: 30/04/2022