Swali: Namweka alama ngamia kwenye shavu na nikimwacha na nikimweka alama mahali pengine nakhofia nikaweka alama ya kabila ya mnyama mwingine, kwa sababu kila kabila la mnyama lina mahali pa alama yake. Ni ipi hukumu?

Jibu: Haijuzu kuweka alama usoni. Haijuzu kuweka alama usoni. Haijuzu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza jambo hilo. Amekataza kuweka alama usoni. Hata hivyo aweke alama mahali pengine inayotofautiana na alama za watu. Ni sawa akaweka alama mikononi, mapajani na masikioni. Kuhusu usoni haifai.

Swali: Ni upi mpaka wa uso?

Jibu: Uso unatambulika. Mahali pa pua, mdomo na macho mawili. Kuhusu masikio sio sehemu ya uso. Masikio ni sehemu ya kichwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23188/حكم-الوسم-على-وجه-الحيوان
  • Imechapishwa: 23/11/2023