Safari kwa ajili ya ulinganizi na kuiacha familia nyuma

Swali: Je, ni jambo linalokubalika katika Shari´ah kuwaacha familia na kusafiri kwa ajili ya kuifanya upya imani?

Jibu: Afanye kile chenye manufaa makubwa zaidi. Hapana neno akasafiri ikiwa kusafiri kwake hakuwadhuru. Ikiwa kusafiri kwake kunawadhuru basi kupambana na familia yake ndio bora zaidi katika kuwafunza, kuwaelekeza, kuwaongoza na kuchelea juu yao kutokana na shari. Hata hivyo hapana neno ikiwa kusafiri kwake hakuwadhuru na yuko na mtu ambaye atabaki mahali pake au mama yao ni mwema na ataziba pengo lake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23190/حكم-ترك-الاهل-والخروج-لتجديد-الايمان
  • Imechapishwa: 23/11/2023