“Kuna viyoyozi na mafeni na hivyo hakuna haja ya kuchelewesha Dhuhr”

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika joto kali unatokamana na mvuke wa Jahannam. Kukiwa na joto kali basi  pateni baridi kwa swalah.”[1]

Leo kuna wanaosema kwamba kuna viyoyozi na hivyo hakuna haja ya kupata baridi kwa swalah.

Jibu: Hapana. Ni lazima kutendea kazi Sunnah kwa sababu barabara zinakuwa na joto. Sio kila mtu ana kipozeo. Sunnah inatakiwa kufanyiwa kazi na wala haitakiwi kuipoteza na kuipuuza kwa sababu ya madai haya. Kunapokuwa na joto kali basi watu wanatakiwa kupata baridi kwa swalah. Hivo ndivo alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hukumu ni hiyohiyo kuchelewesha ´Ishaa pia ikiwa watu hawajakusanyika wote na wakapenda kuichelewesha. Wakichelewa basi waicheleweshe, na wakiwahi waitangulize. Ni amri ya lazima kuchunga yale aliyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] al-Bukhaariy (535).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23187/حكم-الابراد-بصلاة-الظهر-في-وقتنا-الحالي
  • Imechapishwa: 23/11/2023