Swali: Kuna msikiti nimemuona mtu akimwamsha mwenzake karibu yake wakati Khutbah ikiendelea. Je, anapata dhambi?

Jibu: Hapana, amwamshe kwa mkono na si kwa kuzungumza.

Swali: Ndio, amemwamsha kwa mkono.

Jibu: Hapana vibaya. Ni kama mfano wa ambaye anazungumza akamwashiria anyamaze. Kuashiria kunafaa hata ikiwa ndani ya swalah. Swalah ni tukufu zaidi. Ni sawa mtu akimwashiria mwenzake ima asogee mbele au arudi nyuma kidogo.

Swali: Wakati wa Khutbah au mwishoni mwa safu kikawaida kunakuwepo watoto ambapo mtu anawasikia wanazungumza. Je, awaashirie?

Jibu: Awaashirie. Hapana vibaya.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22056/حكم-الاشارة-باليد-للتنبيه-اثناء-خطبة-الجمعة
  • Imechapishwa: 21/10/2022