Swali: Shaykh! Kuwaamini watu wema ni miongoni mwa shirki kubwa. Sisi tunaishi kwenye kijiji ambapo kumejaa Suufiyyah na kuwaamini watu wema, Tawassul na kumuomba uokovu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni ipi hukumu ya kumuombea du´aa yule mwenye kufa miongoni mwa mababu zetu na wengineo na hii ndio hali yake?

Jibu: Nimekwambia kuwa, yule mwenye kufa katika shirki, usimuombee du´aa. Ama ambaye alikuwa tu na maasi na dhambi ambazo ni chini ya dhirki, muombee du´aa na msamaha.

Ni juu yenu kuilingania jamii hii katika dini ya Allaah, wawekeeni wazi na muwanasihi. Huu ni wajibu wenu. Huu ndio wakati mnaohitajika. Wabainishieni. Msiwakalie kimya na mkakata tamaa juu ya kuongoka kwao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (50) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-6-10.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020