Mume anataka mke atoke na mavazi ya mapambo

Swali: Ni ipi nasaha yako kwa mume anayemwamrisha mke wake avae mavazi ya mapambo na ya kuvutia pindi anapotoka nje ya nyumba yake?

Jibu: Huyu anaamrisha maovu na anakataza mema. Hii ni sifa ya wanafiki. Kutoka hali ya kuwa amejipamba, haya ni maovu. Anaamrisha maovu. Ni wajibu kwake kutubu kwa Allaah (´Azza wa Jall). Badala yake amwamrishe kujisitiri, kujiheshimisha na kuwa na hayaa wakati wa kutoka.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (52) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-10-18.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020