Swali: Bwana mmoja yuko na ngamia wazuri na wa bei ghali. Je, inafaa kwake kumnunua ngamia wa kawaida na akamtoa zakaah kwa ajili ya wale ngamia wale ghali?

Jibu: Anatakiwa kumtoa zakaah ngamia wa kati na kati, asiwe wa bei ya ghali sana wala wa bei nafuu. Ikiwa mali yake imechanganyika kati ya mali nzuri na mali mbaya, basi anatakiwa kuitolea zakaah kwa ile ambayo ni kati na kati. Ama ikiwa mali yake yote ni nzuri, basi anatakiwa kutoa zakaah katika ile nzuri. Ikiwa mali yake yote ni mbaya, basi anatakiwa kutoa zakaah katika ile mbaya. Na ikiwa mali yake yote ni kati na kati, basi anatakiwa kutoa zakaah katika ile ya kati na kati.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (16)
  • Imechapishwa: 24/04/2021