Zakaah juu ya kondoo na mbuzi wa matumizi binafsi

Swali: Kuna mtu ana wanyamahoa ambapo anakula katika nyama yake na anakunywa katika maziwa yake. Anapokuja mtu kutaka kununua, basi anamuuzia. Je, niwatolee zakaah kwa njia ya bidhaa ya biashara au mifugo?

Jibu: Watazingatiwa kutolewa zakaah ya mifugo wakiwa wako nje na kuchungwa kupewa malisho kusikopungua muda wa miezi sita. Kwa hivyo hawazingatiwi kutolewa zakaah ya mifugo. Hawatolewi zakaah ikiwa wewe mwenyewe ndiye unawalisha. Lakini ukiwauza na ukapata pesa na pesa hiyo ikazungukiwa na mwaka, katika hali hiyo utaitolea zakaah pesa hiyo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (16)
  • Imechapishwa: 24/04/2021