35. Mfungaji kukhitimisha Qur-aan ni jambo la lazima?

Swali 35: Mfungaji kukhitimisha Qur-aan katika Ramadhaan kunazingatiwa ni jambo la lazima?

Jibu: Mfungaji kukhitimisha Qur-aan katika Ramadhaan sio jambo la lazima. Lakini mtu katika Ramadhaan anatakiwa kusoma Qur-aan kwa wingi. Hiyo ndio ilikuwa Sunnah ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Jibriyl alikuwa akimfunza (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Qur-aan kila Ramadhaan.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 48 mas-alatu fiy Swiyaam, uk. 32
  • Imechapishwa: 24/04/2021