Swali: Mamangu ni kafiri. Inajuzu kwenda kumtembelea nyumbani kwake?

Jibu: Ndio. Mzazi ana haki yake hata kama atakuwa kafiri. Haki ya mzazi ni kutendewa wema na kutunzwa vizuri. Usifuate dini yake:

وَإِن جَاهَدَاكَ عَلَىٰ أَن تُشْرِكَ بِي مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ فَلَا تُطِعْهُمَا

“Lakini [wazizi wawili] wakikufanyia juhudi kwamba unishirikishe na yale usiyokuwa na elimu nayo, basi usiwatii.” (31:15)

Usiwatii katika mambo ya dini. Ama kuhusu kuwatunza vizuri na kuwatendea wema ni katika aina ya kulipiza wema.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (35) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighasah%20%20-%2017-%2010-1436.mp3
  • Imechapishwa: 12/02/2017