Swali: Je, anaswaliwa mtu ambaye amekufa akiwa na deni?
Jibu: Aswaliwe na alipiwe deni lake.
Swali: Alikuwa na uwezo lakini hakutekeleza…
Jibu: Hata kama. Anatakiwa kuswaliwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliacha kuwaswalia pale mwanzoni [mwa Uislamu] kasha baadaye akasema:
”Mswalieni mwenzenu.”
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22268/هل-يصلى-على-من-توفي-وعليه-دين
- Imechapishwa: 21/01/2023