Kumsusa mtu mwenye kuacha swalah

Swali: Je, inajuzu kumsusa mtu asiyeswali katu hata kama atakuwa ni kaka yangu?

Jibu: Ndio. Yule ambaye anakusudia kuacha swalah, huyu sio muislamu:

لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ

“Hutopata watu wanaomuamini Allaah na siku ya Mwisho kwamba wanawapenda wale wanaopinzana na Allaah na Mtume Wake, japo wakiwa ni baba zao, au watoto wao, au ndugu zao.” (58:22)

Check Also

Si kwamba inajuzu, bali ni wajibu kuomba talaka!

Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke kuomba kujivua katika ndoa kutoka kwa mume wake ikiwa anapuuzia …