Kijana asiyeweza kuoa akivumilia ana thawabu?

Swali: Mimi ni kijana sina uwezo wa kuoa kutokana na hali ya kifedha. Je, nina thawabu kwa kusubiri kwangu juu ya jambo hili?

Jibu: Ndio. Usisahau maneno ya Allaah (Ta´ala):

وَلْيَسْتَعْفِفِ الَّذِينَ لَا يَجِدُونَ نِكَاحًا حَتَّىٰ يُغْنِيَهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ

“Wajizuie na machafu wale ambao hawapati uwezo wa ndoa mpaka Allaah awatajirishe katika fadhilah Zake.” (24:33)

Akifanya aliyomuamrisha Allaah ana ujira.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/15082
  • Imechapishwa: 20/09/2020