Mke wangu anataka kusafiri kumuuguza mamake bila Mahram

Swali: Mke wangu anataka kusafiri kwenda mji mwingine kwa kuwa mama yake ni mgonjwa. Mimi namkataza hilo kwa kuwa anataka kusafiri peke yake. Je, inafaa kwangu kumkataza Kishari´ah?

Jibu: Ni wajibu kwako kumkataza Kishari´ah. Ni wajibu. Usimuache akasafiri peke yake. Si halali kwake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Si halali kwa mwanamke anayemwamini Allaah na Siku ya Mwisho kusafiri bila ya kuwa pmoja naye Mahram.”

Si halali kwake. Mkataze juu ya kitu ambacho sio halali. Lakini chuma thawabu kwa kusafiri pamoja naye na huku ukihesabu kupata ujira. Safiri pamoja naye hata kama utapata tabu na madhara kidogo, kuwa ni mwenye subira.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/15082
  • Imechapishwa: 20/09/2020