Kumsifu Allaah kabla ya kuomba du´aa

Swali: Hadiyth ya Faadhwalah inayosema:

“Anapoomba du´aa mmoja wenu, basi aanze kumsifu Mola wake.”

Je, hilo ni kwa njia ya ulazima au mapendezo?

Jibu: Kilichotangaa kwa wanazuoni ni kwa kwamba inapendeza kwa muumini. Ni miongoni mwa adabu za kuomba du´aa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23016/هل-البدء-بالحمد-في-الدعاء-واجب-ام-مستحب
  • Imechapishwa: 13/10/2023