Swali: Baadhi ya watu wanamtia aibu maiti.

Jibu: Haijuzu. Kumsengenya maiti ni kubaya zaidi kuliko kumsengenya aliye hai. Hapa ni pale ambapo jambo ni lenye kujificha. Lakini [ni sawa ikiwa ni] kitu kilicho dhahiri ambacho malengo ya mtu ni kukitahadharisha, kwa sababu watu wanamwigiliza ambapo mtu akabainisha kuwa jambo hilo halijuzu na kwamba haijuzu kumfuata mtu fulani katika Bid´ah au maasi yake yaliyo dhahiri.

Swali: Vipi kwa mlinganizi anayelingania katika shari?

Jibu: Ndio, jambo ambalo mtu anachelea akafuatwa na wengine katika shari hiyo. Shari iliyo waziwazi.

Swali: Vipi ikiwa shari yake ni yenye kufupika naye?

Jibu: Ikiwa shari yake ni yenye kujificha na haiko dhahiri, mtu asiipeleleze.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23436/ما-حكم-غيبة-الميت
  • Imechapishwa: 21/01/2024