51. Hadiyth ”Peponi kuna sehemu ya kukaa… ”

51 – Muhammad ametuhadithia: ´Abdullaah bin Ja´far ametuhadithia: ´Abdur-Rahmân bin Muhammad bin ´Abd al-Qaariy amenikhabarisha, kutoka kwa ´Awn bin ´Abdillaah, ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

إن في الجنة مجلساً لم يعطه أحد قبلي، وأنا أرجو أن أعطاه، فسلوا الله لي الوسية

”Peponi kuna sehemu ya kukaa ambayo hakupewa yeyote kabla yangu. Nataraji nitapewa nayo mimi. Niombeeni kwa Allaah Njia (الوسية).”[1]

[1] Cheni ya wapokezi ni dhaifu, lakini maana ya Hadiyth inaafikiana na iliotangulia.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 52
  • Imechapishwa: 21/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy