50. Hadiyth ”Yule mwenye kuniswalia… ”

50 – Muhammad bin Abiy Bakr ametuhadithia: ´Umar bin ´Aliy ametuhadithia, kutoka kwa Abu Bakr al-Jashmiy, kutoka kwa Swafwaan bin Sulaym, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Amr, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

من صلى عليَّ أو سأل لي الوسيلة، حقت عليه شفاعتي يوم القيامة

”Yule mwenye kuniswalia au akaniombea Njia (الوسيلة), basi utamstahikia uombezi wangu siku ya Qiyaamah.”[1]

[1] Swahiyh. Wapokezi wa cheni yake ni waaminifu isipokuwa tu ´Umar bin ´Aliy, licha ya uaminifu wake, alikuwa akifanya udanganyifu mbaya. Alikuwa akisema ”Nimesikia” au ”Tumehadithiwa” kisha baadaye anayamaza kitambo halafu kwa mfano anasema ”Hishaam bin ´Urwah” na ”al-A´mash”. Mtu kama huyu hazitakiwi kukubaliwa Hadiyth zake ijapo atamsema wazi aliyemsimulia. Hata hivyo nimewaona wanazuoni wakizikubali Hadiyth zake anaposema kwa uwazi ”Tumehadithiwa” Hata miongoni mwa wale waliomtuhumu kwa udanganyifu wake huo, katika hali hii ni Ibn Sa´d, amesema baada ya kumtuhumu kwake kwa jambo hilo:

”Alikuwa ni mtu mwema. Hakuna ambacho walikuwa wakimkosoa zaidi ya udanganyifu wake. Hakuna kingine. Sikuwa nakubali chochote kutoka kwake mpaka amtaje ni nani amemuhadithia.”

Sijui namna ya ufikiriaji wake. Abu Bakr al-Jashmiy jina lake ni ´Iysaa bin Tahmaan na ni mwenye kuaminika, ingawa Ibn Hibbaan alimfanya kuwa ni somo la ukosoaji usiokuwa na msingi. Sababu ya ukosoaji unatokana na wengine, ndivo alivosema Haafidhw Ibn Hajar katika “at-Taqriyb”.

Hata hivyo Hadiyth ni Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 51
  • Imechapishwa: 21/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy