49. Hadiyth ”Hakika Njia ni ngazi… ”

49 – Ishaaq bin Muhammad[1] al-Farwiy ametuhadithia: Ismaa´iyl bin Ja´far ametuhadithia, kutoka kwa ´Umaarah – naye ni Ibn Ghaziyyah – kutoka kwa Muusa bin Wardaan, aliyesimulia kuwa amemsikia Abu Sa´iyd al-Khudriy akieleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

إن الوسيلة درجة عند الله ليس فوقها درجة، فسلوا الله أن يؤتيني الوسيلة على خلقه

”Hakika Njia ni ngazi mbele ya Allaah ambayo hakuna ngazi ilio juu yake. Niombeeni kwa Allaah anipe Njia juu ya viumbe Wake.”[2]

[1] Katika ile ya asili imekuja ”Muhammad bin Ishaaq bin Muhammad”, jambo ambalo ni kosa.

[2] Cheni ya wapokezi ni nzuri.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 50
  • Imechapishwa: 21/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy