Hukumu ya anayeendelea kunywa pombe baada ya kupigwa bakora mara tatu

Swali: Je, mnywa pombe ikiwa anadumu kunywa pombe anauliwa?

Jibu: Kinachotambulika kwa wanazuoni ni kwamba anatekelezewa adhabu ya Kishari´ah. Kila kunapothibiti kwake anatekelezewa adhabu. Baadhi ya wanazuoni wengine wakaona kuwa mara ya nne na baada ya hapo anatakiwa kuuliwa. Hata hivyo wanazuoni wengi wanaona kuwa anatakiwa kutekelezewa adhabu mpaka anyooke sawasawa. Hilo ni kutokana na kisa cha yule bwana ambaye alikuwa akiletwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo akimsimamishiwa adhabu. Mtu mmoja akasema: “Ni mara ngapi ameletwa kwake. Allaah amtweze!” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamkemea.

Swali: Hadiyth iliyopokelewa ndani yake ya kwamba anatakiwa kuuliwa mara ya nne?

Jibu: Imesahihishwa na kikosi cha wanazuoni kupitia kwa Mu´aawiyah. Ni kwa njia ya kumuaziri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23435/حكم-المدمن-على-الخمر-بعد-جلده-ثلاث-مرات
  • Imechapishwa: 21/01/2024