Kumpenda mke mmoja zaidi kuliko mwingine

Swali: Kabla ya mume kufa mke amemsamehe mume wake kwa sababu ya kuegemea kwake kwa mke mwingine. Je, atakuja siku ya Qiyaamah hali ya kuwa bega lake moja limepinda[1] au Allaah amekwishamsamehe?

Jibu: Sio kumili huko kulikokusudiwa. Hawezi kuwa mwadilifu inapokuja katika suala la mapenzi:

وَلَن تَسْتَطِيعُوا أَن تَعْدِلُوا بَيْنَ النِّسَاءِ وَلَوْ حَرَصْتُمْ

“Wala hamtoweza kufanya uadilifu kati ya wake japokuwa mtatupia.”[2]

Bi maana katika mapenzi. Ama kufanya uadilifu katika matumizi, mavazi, kugawa zamu usiku na makazi kunamlazimu. Kuna uadilifu unaowezekana, uadilifu usiowezekana.

[1] Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Ambaye yuko na wake wawili na akaegemea kwa mmoja wao, basi atakuja siku ya Qiyaamah hali ya kuwa bega lake moja limepinda.” (Abu Daawuud (2133), at-Tirmidhiy (1141) na Ibn Maajah (1969)).

[2] 4:129

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (41)
  • Imechapishwa: 30/11/2023