Swali: Je, inafaa kwa muislamu kula tamtam zilizo na mafuta ya nguruwe?

Jibu: Kamwe. Haijuzu. Vitu vilivyo na mfuta ya nguruwe haviliwi.

Swali: Je, inafaa kwake kuvila ikiwa mafuta hayo ya nguruwe yamekwishayayuka?

Jibu: Hakuna tamtam nyingine? Asisogelee nguruwe wala kitu kilicho na nguruwe, kwa sababu ni mchafu. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

أَوْ لَحْمَ خِنزِيرٍ فَإِنَّهُ رِجْسٌ

”… au nyama ya nguruwe – kwani hiyo ni uchafu… ”[1]

[1] 6:145

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (41)
  • Imechapishwa: 30/11/2023