392 – Mutwarrif ameeleza:

“Niliikaa na kundi kutoka katika Quraysh, ambapo akaja bwana mmoja na akaanza kuswali na kurukuu na kusujudu bila kukaa chini. Nikasema: “Naapa kwa Allaah! Sifikirii kama huyu anajua kama atamaliza kwa shufwa au witr.” Wakasema: “Kwa nini usisimame ukamwambia?” Nikasimama na kusema: “Ee mja wa Allaah! Sifikirii kama unajua kuwa unatakiwa kumaliza kwa shufwa au witr.” Akasema: “Lakini Allaah anajua. Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

مَن سجدَ لله سجدةً؛ كَتَبَ اللهُ له بها حسنةً، وحَطَّ عنه بها خطيئةً، ورفع له بها درجةً

“Yule mwenye kumsujudia Allaah sijda, basi Allaah atamwandikia kwayo jema, atamfutia kwayo kosa na atamnyanyua kwayo ngazi.”

Nikasema: “Wewe ni nani?” Akasema: “Abu Darr.” Nikawarudilia wenzangu na kusema: “Allaah akulipeni shari! Mmeniamrisha kumfunza mmoja katika Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)!”[1]

Imekuja katika upokezi mwingine:

“Nikamuona jinsi anavyorefusha kusimama na akirukuu na kusujudu kwa wingi. Nikamtajia jambo hilo, ambapo akasema: “Nafanya vizuri kadri niwezavyo. Hakika mimi nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

من ركَع ركعةً، أو سَجَدَ سجدةً؛ رُفع له بها درجةً، وحُطَّ عنه خَطيئةً

“Yule mwenye kurukuu Rukuu´ au akasujudu sijda, basi humnyanyua kwayo ngazi na akamfutia kwayo kosa.”[2]

Ahmad na al-Bazzaar wamepokea mfano wake. Kutokana na mkusanyiko wa njia zake ni nzuri au pengine hata Swahiyh.

[1] Swahiyh kupitia zingine.

[2] Swahiyh kupitia zingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/280)
  • Imechapishwa: 30/11/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy