Kumpeleleza anayetaka kuingia katika Uislamu

Swali: Kuna mwindonesia anayetaka kuingia katika Uislamu. Je, watu wana haki ya kumfanyia taratibu za kusilimu au wahakikishe juu ya hali yake?

Jibu: Inatakiwa kufanya haraka kumsaidia, kumfanya kuwa na shauku ya Uislamu, kumpendezesha na kumrahisishia jambo lake kwa ajili ya kushirikiana katika wema na kumcha Allaah.

Swali: Kwa hivyo watu wasikague nia?

Jibu: Hapana, jambo lake aachiwe Allaah. Anatakiwa kujengewa dhana njema kwa ajili ya kumtia moyo wa kuingia katika Uislamu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22898/هل-يجب-التحقق-من-قصد-من-اراد-ان-يسلم
  • Imechapishwa: 14/09/2023