Kukusanya nia ya deni la Ramadhaan na siku sita za Shawwaal

Swali: Je, inafaa kwa mtu kukusanya nia ya kufunga siku sita za Shawwaal na kulipa deni analodaiwa la Ramadhaan katika masiku haya sita kwa nia ya kulipa na akapata ujira wa yote mawili au ni lazima alipe deni kwanza ndio alipe zile siku sita za Shawwaal?

Jibu: Anatakiwa kulipa deni kwanza kisha ndio alipe siku sita akitaka kufanya hivo. Siku sita hizi zimependekezwa. Akilipa katika Shawwaal zile siku anazodaiwa kisha akafunga siku sita hizi ndani ya mwezi wa Shawwaal ni kheri kubwa. Lakini kufunga siku sita kwa kunuia deni na siku sita hainidhihirikii kuwa anapata thawabu za siku sita za Shawwaal. Swawm ya siku sita inahitajia nia maalum katika masiku mengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/12597/هل-يجوز-صيام-ست-من-شوال-بنية-القضاء-والتنفل
  • Imechapishwa: 07/05/2022