Kufunga Rajab, Sha´baan, Ramadhaan na siku sita za Shawwaal

Swali: Shari´ah inasemaje juu ya kufunga miezi mitatu; Rajab, Sha´baan na Ramadhaan na siku sita za mwezi wa Shawwaal kwa sura endelevu pamoja na kuzingatia kwamba mimi nina uwezo wa kufanya hivo?

Jibu: Hapana neno kufanya hivo. Hapana neno kufanya hivo. Hapana vibaya kwa ambaye atafunga mwezi wa Rajab, Sha´baan na Ramadhaan. Kilichochukizwa ni kufunga Rajab peke yake ambapo akaipwekesha kwa funga. Hata hivyo ni sawa endapo ataifunga na Sha´baan.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/13003/حكم-صوم-رجب-وشعبان-ورمضان-والست-من-شوال
  • Imechapishwa: 07/05/2022